BY ISAYA BURUGU 30TH MARCH,2023-Makabiliano kati ya polisi na wandamanaji yameshuhudiwa katika eneo la Mathare number 10 mapema leo  katika siku ya pili ya mandamano ya mungano wa Azimio la Umoja juma hili.Mandamano ya leo yameashiria raundi ya tatu ya mandamano ya kupinga serikali yanayonggozwa na kinara wa Azimio Raila Odinga kupinga gharama ya juu ya kimaisha nchini  sawa  na kutofungua sava za uchaguzi mkuu wa mwaka jana mojawapo ya matakwa ya Odinga.

Hata hivyo mandamano hayo yanasalia kinyume cha sharia kwa mjibu wa notisi  kutoka kwa Waziri wa usalama wa ndani Kithure kindiki .Kupitia notisi hiyo aliyoitoa jana ,Waziri KIndiki amewaonya wakenya wote dhidi ya kushiriki mandamano hayo akisema watakuwa wanavunja sheria.Waziri alitaja ghasia zilizoshuhudiwa katika muda wa majuma mawili yaliyopita ambapo mandamano hayo yameandaliwa ,kama sababu za kupiga marufuku mandamano yenyewe.

 

Wakati huo huo Kuna uwepo mkubwa wa polisi wa kupambana na ghasia kwenye njia nyingi za kuingia na kutoka katika jiji la Nairobi.Barabara karibu na Ikulu zimewekwa vizuizi huku polisi wakiwakagua madereva ambao wanazitumia.Maafisa hao walitumwa usiku wa kuamkia leo .Hali ni kama hiyo kwenye miji mingine mikuu siku ya mandamano .

Polisi wametakiwa kutotumia nguvu kupita kiasi wanaposhughulikia maandamano hayo.Hadi sasa watu wanne wameuawa, watano wamejeruhiwa na mali nyingi imeharibiwa katika maandamano mawili yaliyopita nchini.Shule nyingi jijini zilitangaza kuwa hakutakuwa na mafunzo hivi leo  Machi 30 kutokana na maandamano yaliyopangwa.

Shirika la Reli la Kenya lilitangaza kuwa hakutakuwa na huduma za  kusafirisha abiria kwa sababu ya maandamano.Magari mengi ya huduma za umma pia yameondoka barabarani kwa hofu kwani biashara nyingi zimefungwa pia.

Kule Jijini Kisumu, maduka mengi yameonekana kufungwa huku kukiwa na shughuli chache tu zinazoendelea leo.Barabara nyingi kuu za mji huo pia zimesalia na watu wachache tu .

 

 

 

March 30, 2023