Maafisa wa polisi kutoka kaunti ndogo ya Narok Mashariki, walifanikiwa kulikabili kundi la watu ambalo lilikua likitekeleza uhalifu na kuharibu mali katika shamba la Kedong mpakani mwa kaunti ndogo za Narok Mashariki na Naivasha.

Taarifa zinaeleza kwamba maafisa hao waliokuwa katika shughuli zao za doria, walifanikiwa kuwatawanya vijana waliokuwa wamelivamia shamba hilo la ekari 75,000 na kusimamisha shughuli Zaidi za uharibifu ambazo zinahusisha ubomoaji wa ua linalozingira shamba hilo.

March 30, 2023