BY ISAYA BURUGU,29TH APRIL,2023-Polisi hivi leo wamewaokoa watu 17 kutoka kwa kanisa linaloshukiwa kuwa la mafunzo ya kupotosha huko Nakuru.Polisi wanasema , mzazi kutoka Kaunti ya Uasin Gishu aliripoti kuwa bintiye alikuwa amefungiwa katika nyumba moja katika kijiji cha Kamwene ‘B’, wadi ya Kihingo na Kaunti Ndogo ya Njoro.

Polisi walisema kazi hiyo ilikusudiwa kwa bintiye mwenye umri wa miaka 35 ambaye ni mama wa watoto wanne.Kwa mujibu wa taarifa hizo, mwanamke huyo alitakiwa kuripoti Aprili 26, 2023, lakini alikataa na kusafiri na mumewe hadi kijiji cha Kamwene ‘B’.Polisi waliwapata wakiwa wamezuiliwa katika nyumba moja ambayo ni ya mwanamke anayeshukiwa kuendesha kanisa lisilosajiliwa na linaloshukiwa kuwa la itikadi potovu linalojulikana kama ‘Army Rurwama’.

Wote waliokolewa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Njoro kwa uchunguzi zaidi.

Wale 17 wanasemekana kufanyiwa maombi na kufunga.Watu hao 17 waliokolewa huku kukiwa na uchunguzi kuhusu kifo cha zaidi ya watu 100 katika msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi.

 

April 29, 2023