BY ISAYA BURUGU,1ST APRIL,2023-Pombe imetajwa kuwa dawa ya kulevya inayotumika sana nchini,vijana wengi wakisemekana kuadhirika Zaidi na matumizi ya pobe eneo la pwani.

Haya ni kwa mjibu wa afisa wa elimu ya umma kwenye shirika la kukabiliana na matumizi ya pombe na mihadarati NACADA Lucy Wairimu anasema waraibu wa pombe hiyo huadhirika Zaidi kiafya na kimwili. Akizungumza eneo  bunge la likoni kaunti ya Mombasa,Wairimu amezitaja kaunti za Kilifi na Mombasa kama zilizoadhirika Zaidi huku vijana wengi Kilifi wakitumia pombe yam nasi.

Wairimu amesema hali hiyo inatokana na dhana potovu kuwa pobe asilia haina madhara.Pia amewataka wafanyibiashara wa pombe kuendesha biashara hiyo mbali na Watoto.

 

 

 

 

 

April 1, 2023