TAANZIA!
Papa mstaafu Benedict XVI ameaga dunia. Taarifa kutoka katika Makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Vatican zimedhibitisha kuwa papa Mstaafu Benedict XVI aliaga dunia mwendo wa saa tatu asubuhi ya leo katika makaazi yake kwenye Monasteri ya Mater Ecclesiae kule Vatican akiwa na umri wa miaka 95.

Papa Benedict aliyezaliwa katika taifa la ujerumani 16 April 1927 alihudumu kama papa kuanzia tarehe 19 April 2005 na kustaafu tarehe 28 February 2013 kutokana na sababu za kiafya.

Papa Benedict XVI ambaye jina lake asili ni Joseph Ratzinger alikuwa mkuu wa kusanyiko la makadinali kote duniani, kabla ya uteuzi wake kuwa papa mwaka wa 2005 baada ya kifo cha mtangulizi wake Papa Yohane Paulo wa II. Baadhi ya mambo yanayohusishwa sana na Maisha ya Papa Benedict ni Pamoja na mafunzo yake kuhusu umuhimu w akutambua mapenzi ya Mungu Pamoja na msimamo wake katika kulitetea kanisa katoliki.

Hali ya papa mstaafu imekua ikidorora katika siku kadhaa zilizopita, na kabla ya kutangazwa kwa taarifa za mauko yake, papa Francis alikua ametoa rai kwa waumini kuendelea kumwombea Papa huyo.

Na huku viongozi mbalimbali wa kidini wakianza kutoa jumbe za rambirambi baada ya kifo cha Papa Mstaafu Benedict XVI, makao makuu ya kanisa katoliki mjini Vatican yamesema kuwa kiongozi wa kanisa katoliki dunianai Papa Francis ataadhimisha Misa ya mazishi ya Papa Mstaafu Benedict XVI katika uwanja wa St.Peters Square siku ya Alhamisi. Ibada hii ni baadhi ya matukio ya Nadra Zaidi katika hoistoria ya kanisa katoliki, ambapo Papa mmoja atakua anaongoza misa ya aina hii kwa papa mwenzake.

Taarifa Zaidi zimeweka wazi kuwa Kuanzia Jumatatu asubuhi, tarehe 2 Januari 2023, mwili wa Papa Mstaafu utakuwa katika Basilica ya Mtakatifu Petro ili kutoa nafasi kwa waumini kutoa heshima za mwisho.

Taarifa zidi kutoka VATICAN NEWS

December 31, 2022