Kinara wa upinzani Raila Odinga amefutilia mbali taarifa kuwa kulikua na mkutano kati yake na Rais William Ruto kabla ya tangazo la kusitisha maandamano siku ya Jumapili.
Odinga ambaye alihutubia waandishi wa habari kabla ya mkutano wa wajumbe wa muungano wa Azimio hio kesho amesema hakuandaa kikao cha aina yoyote na Rais Ruto, ila ameeleza baadhi ya wanachama wa muungano wa Upinzani walikutana na wawakilishi wa serikali kabla ya kuafikiwa kwa makubaliano haya.
Odinga aidha ameongeza kwamba upande wa serikali ulitoa pendekezo ambalo liliendana na matakwa yao, na hivyo wakaamua kutangaza masharti ya kutafta suluhu kuhusu suala la utata wa uteuzi wa makamishena wa tume ya IEBC.
Odinga aidha ameweka peupe kwamba muungano wake hauna nia yoyote ya kuandaa mashauriano yoyote ya kuingia serikalini, akitangaza kwamba semi kuhusiana na maswala ya Handsheki yanasukumwa na viongozi wa mrengo tawala.