MAZUNGUMZO

Kinara wa Upinzani nchini Raila Odinga, sasa anasema kwamba viongozi kutoka upande wa serikali wamekataa kujihuisha katika aina yoyote ya mazungmo na upinzani ili kutafuta suluhu kuhusu mgogoro uliopo kati ya pande hizi mbili.

Odinga aliyezungumza mapema leo, amefichua kuwa Rais wa taifa Jirani la Tanzania Samia Suluhu Hassan alikuwa humu nchini majuma mawili yaliyopita kwa nia ya kuongoza mazungumzo kati ya serikali na Upinzani, jambo ambalo upande wa viongozi wa serikali walikataa kutimiza.

Odinga ameeleza kwamba yeye na viongozi wengine wako radhi kutafuta mwafaka kuhusu hali ya maisha ya wakenya humu nchini kwa sasa, huku akiikosoa serikali kwa kuyafumbia jicho malalamishi yao.

 

July 25, 2023