Kiongozi wa Azimio la umoja Raila Odinga ametoa matakwa kumi kwa Rais William Ruto kuhusu Mswada wa Fedha wa 2023.
Raila sasa anamtaka Ruto akome kuwalemea Wakenya na badala yake azingatie kupunguza gharama ya maisha.
Akizungumza jijini Nairobi Raila pia amemtaka Ruto kupitisha bajeti isiyo na msingi na kuacha kuchukua bajeti ya awali kama msingi. Raila alisema kuwa kila bajeti lazima ianzie sufuri ambapo kila kitu lazima kihalalishwe.
Aidha ameonya kuwa iwapo Rais Ruto atabatilisha Bunge la Kitaifa kuhusu Mswada wa Fedha wa 2023, nao pia watajipanga upya na kumshinda.
Ameongeza kuwa serikali imekosa sababu za kueleza ni kwa nini Mswada huo lazima upitishwe Bungeni.
Rather than burden Kenyans, we want Ruto to undertake the following:
1. Stop duplication of county roles and responsibilities. In the proposed Bill, budget for health is growing by Ksh35 billion at the national level, yet health is a devolved functions.
2. Adopt zero-based…
— Azimio TV (@AzimioTv) June 8, 2023
No regime has imposed so many high taxes on our people in return for nothing except fantasies and fairy tales. This Bill is economic sabotage.
If Ruto insists on this Bill, this country will go into full recession. This Bill requires and must get fierce resistance. pic.twitter.com/rC9buuJikT
— Raila Odinga (@RailaOdinga) June 8, 2023