Kinara wa upinzani Raila Odinga amepinga mapendekezo yaliyo katika mswada unaopendekezwa wa ukusanyaji ushuru nchini. Odinga amesema kwamba mswada huo unafaa kuangaziwa upya kutokana na mambo mengi anayoeleza kuwa hayajawekwa wazi kwa wakenya.
Akizungumza jijini Nairobi siku ya Jumatatu, Odinga ameeleza kwamba atapinga mswada huo kutokana na mzigo wa ushuru ambao utaelekezwa kwa Wakenya iwapo mswada wenyewe utaidhinisha. Katika taarifa yake, kinara huyo wa muungano wa Azimio la Umoja amepinga pendekezo la Kutozwa asilimia 3 ya mshahara kwa wafanyakazi wa umma kwa ajili ya kuwapa nyumba za bei nafuu, akieleza kwamba hii ni njama ya serikali kukopa fedha kwa wakenya bila ya kutaka kulipa riba kwa mikopo hii.
Aidha pia amepinga pendekezo la kuwatoza ushuru wa asilimia 15 kwa watu wanaojihusisha na video kwenye mitandao ya kidijitali.
Kuhusiana na mazungumzo ya pande mbili kati ya serikali na upinzani, Odinga ameeleza kwamba upande wa serikali umeonyesha ajizi na kutokua na umakini katika mazungumzo hayo, Odinga sasa akisema kwamba iwapo mazungumzo hayo hayataong’a hivi karibuni basi watatafuta namna nyingine za kushinikiza mabadiliko.
The proposed Finance Bill by the Kenya Kwanza Regime is a punishing burden on Kenyans. The tsunami of taxes will suffocate the jobless youth and the poor.
We strongly oppose this anti-people budget and will ensure it doesn't pass. If it does, we disassociate ourselves from it. pic.twitter.com/08ekkEZ5Zk
— Raila Odinga (@RailaOdinga) May 8, 2023