BY ISAYA BURUGU 4TH MAY 2023-Rais Wiliam Ruto hivi leo amekuwa mgeni wa katibu mkuu wa umoja wa mataiafa Antonio Guteres katika ikulu ya Nairobi.Guteres akizungumza kwenye kikao hicho amesema kuwa ni jambo la kutamausha kuona kuwa adhari za kikoloni zingali bayana katika mataiafa mengi ya Afrika hivi leo, miaka mingi baada ya mataiafa hayo kupata uhuru Wake

.Katibu huyo mkuu wa umoja wa mataiafa akisema wakati umefika kwa bara la Afrika kuwakilishwa vyema katika  miungano na mashirika ya umoja huo kwenye Nyanja za kimataifa ili kuhakikisha kuwa mataiafa ya Afrika yanastawi kama yale yalio n auchumi mkubwa.

Kwa upande wakae Rais Ruto amesema kenya itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kikanda na kimaeneo kama inavyoshuhudiwa kwa sasa nchini DRC ambapo Kenya imetuma majeshi ya kusaidia kurejesha amani.Amemtaka Guteres kuendelea kuunga Kenya mkono katika kuafikia malengo yake.

 

May 4, 2023