Kiongozi wa Taifa, Rais William Ruto, anaondoka nchini leo kwa ziara ya siku tatu katika mataifa ya Comoros na Jamhuri ya Congo. Ziara hii inalenga kuimarisha uhusiano wa Kenya na nchi hizi mbili na kukuza ushirikiano katika masuala ya kiuchumi na kisiasa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Ikulu, Bwana Hussein Mohammed, Rais Ruto atakuwa mgeni wa heshima katika maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru wa taifa la Comoros. Mwaliko huo umetolewa na Rais Azali Assoumani, ambapo Rais Ruto atashiriki katika sherehe za kitaifa za kuadhimisha uhuru huo.
Baada ya ziara hiyo, siku ya Ijumaa Rais Ruto ataelekea Jamhuri ya Congo kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili . Katika ziara hii, Rais Ruto amepangiwa kufanya mazungumzo na Rais Dennis Sassou Nguesso kujadili ushirikiano wa kimkakati kati ya Kenya na Congo. Wawili hao watashughulikia masuala muhimu yanayohusu biashara, uwekezaji, usalama, na ushirikiano wa kikanda.
President @WilliamsRuto departs this evening for a three-day visit to the Union of Comoros and the Republic of Congo. These visits are aimed to strengthen the bilateral ties between the two nations. pic.twitter.com/lu8kvwVyAO
— Hussein Mohamed, MBS. (@HusseinMohamedg) July 5, 2023