BY ISAYA BURUGU,23RD MARCH,2023- Rais William Ruto hivi leo ameshuhudia kuapishwa kwa Makatibu Wakuu 50 wa Tawala katika hafla iliyofanyika Ikulu.Wateule hao wa CAS walitangazwa kwenye gazeti la serikali Jumatano na Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei.

Mawasiliano ya awali kutoka kwa Spika  wa Bunge ,  Moses Wetang’ula alisema kuwa Bunge la  siku ya Jumatano haliwezi kuwahakiki kwa kuwa hakuna kifungu cha kisheria kinachopatia bunge mamlaka ya kuwahakiki.Mawasiliano hayo yaliwekwa wazi na msemaji wa Ikulu, Hussein Mohamed.

Baadhi ya walioapishwa ni pamoja na Mtaalamu wa Mikakati wa Kidijitali Dennis Itumbi, Aliyekuwa Seneta Mteule Millicent Omanga, Aliyekuwa Mbunge wa Starehe Charles Njagua, Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Evans Kidero, Catherine Waruguru (Laikipia Mashariki), Onesmus Ngunjiri (Mbunge wa Bahati), Askofu Margaret Wanjiru ( Seneta wa Nairobi), Isaac Mwaura (Mbunge wa Ruiru) na Rehema Jaldesa (Mwakilishi wa Kike wa Isiolo) miongoni mwa wengine.

Hii ni baada ya mahakama kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na LSK kupinga kubuniwa kwa nafasi hiyo.

March 23, 2023