Rais William Ruto ametoa wito wa kusitishwa vita na makabiliano ya kijeshi katika taifa la Sudan, akieleza kwamba kuendelea kwa hali tata ya kivita katika taifa hilo kunasababisha hali ya wasiwasi sio tu katika taifa hilo bali pia katika ukanda wa mataifa ya IGAD.

Akizungumza katika ikulu ya Nairobi alasiri ya Jumatano 19.04.2023, rais ameeleza haja ya jeshi la Sudan na vikosi vya RSF kusitisha mapigano na uharibifu wa mali, na kuangazia haki msingi za wananchi wa taifa hilo.

Inaelezwa kwamba hadi kufikia sasa watu wapatao 270 wamepoteza Maisha yao kufuatia mapigano hayo.

Rais aidha aliweka bayana kwamba amefanya mazungumzo ya simu na katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kwa nia ya kupata suluhu ya kudumu katika mzozo huo unaoendelea kuchacha katika taifa hilo.

April 19, 2023