Ruto UN

Kiongozi wa taifa Rais William Ruto amependekeza bara la Afrika kutengewa nafasi mbili za kudumu katika baraza la umoja wa mataifa UN, ili kuwezesha bara hili kupiga hatua mbele katika maswala ya maendeleo na pia kuendeleza ajenda yake ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza katika Mkutano wa Wabunge wa bara la Afrika kuhusu Sera ya Hali ya Hewa nchini Afrika Kusini, Ruto ameeleza kwamba baraza la umoja wa mataifa linafaa kuwa na sura inayojumuisha pembe zote za dunia, huku akisema bara la Afrika linafaa kutengewa nafasi mbili za kudumu kwenye baraza lenyewe.

Awali kwenye kikao hicho, Rais Ruto alipata kushtumu hatua ya baadhi ya mataifa mengine nje ya bara hili, kuwadharau viongozi wa Afrika na kutengea muda ambao hauwezi wasaidia hasa katika mikutano na vikao vya kutafuta makubaliano kati ya mataifa hayo na mataifa ya bara la Afrika.

https://twitter.com/WilliamsRuto/status/1658842135171399689?s=20

May 17, 2023