Rais William Ruto amevunja kimya chake, kuhusiana na mapendekezo ya kutozwa kwa asilimia 3 ya mshahara wa wafanyakazi ili kusaidia katika ujenzi wa nyumba za bei nafuu nchini.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa nyumba hizi za bei nafuu katika eneo la South C kaunti ya Nairobi adhuhuri ya leo, rais ameeleza kwamba fedha zitakazotozwa hazitakua sehemu ya ushuru bali ni fedha za wakenya zitakazowekwa katika akiba, pamoja na asilimia tatu itakayotolewa na mwajiri kwa wafanyakazi husika.
Rais ameeleza kwamba waajiri wote watalazimika kuchangia asilimia tatu ya mshara kwa kila mfanyakazi, na kufikisha fedha hizi hadi asilimia sita itakayoelekezwa katika mradi huu wa kuhakikisha kwamba wafanyakazi wanapata mahala pazuri pa kuishi.
Our affordable Housing programme puts the dream of home ownership within the reach of thousands of Kenyans while providing economic opportunities for thousands of others through the construction of the homes. pic.twitter.com/9WnknYSf3C
— William Samoei Ruto, PhD (@WilliamsRuto) May 11, 2023