BY ISAYA BURUGU 30TH JUNE,2023-Rais Wiliam Ruto  ameongoza uzinduzi wa  mpango wa gavamkononi ambao utatoa Zaidi ya huduma alfu 5 za serikali kupitia mtandao wa E-Citizen.

Hatua hiyo inatarajiwa kurahizisha utoaji huduma kwa wananchi na kuwapunguzia safari za kusaka huduma muhimu.

Aidha unatarajiwa kupunguza ufisadi katika afisi za umma.Rais vilevile amezindua mpango mwingine wa Gavana express  ambao unawiana na ule wa vituo vya huduma vya utekelezaji katika kaunti zote nchini.

Ni katika hafla ya uzinduzi huo kwenye jumba la mikutano la KICC jijini Nairobi ambapo rais ametanagza kuwa kuanzia sasa kuelekea siku zijazo fanicha zote zinazotumiwa katika afisi za serikali zitanunuliwa kutoka humu nchini pekee ili kukuza uchumi wan chi.

 

 

 

 

 

June 30, 2023