Rais William Ruto na mkewe, Bi Rachel Ruto, wanatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini Marekani mwezi Mei mwaka huu, kufuatia mwaliko maalum kutoka kwa Rais Joe Biden na mkewe, Bi Jill Biden. Ziara hii imewekwa wazi katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa Mawasiliano wa Ikulu ya White House, Karine Jean-Pierre, siku ya Ijumaa.
Kulingana na taarifa hiyo, kiongozi wa taifa na mkewe wanatarajiwa kuwasili Marekani tarehe 23 mwezi Mei. Ziara hii itakuwa na umuhimu mkubwa katika kudumisha na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na Marekani, hususan ikizingatiwa kuwa mwaka huu unatimiza miaka 60 tangu uhusiano huo kuanzishwa.
Ziara hiyo pia inatarajiwa kuhusisha shughuli mbalimbali za kidiplomasia, ambazo ni sehemu ya juhudi za kukuza ushirikiano kati ya Kenya na Marekani katika masuala ya kiuchumi, kisiasa, na kijamii. Hii itakuwa fursa muhimu kwa viongozi hao kujadiliana masuala ya pamoja na kuimarisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali ya maslahi ya pande zote mbili.
President @WilliamsRuto and First Lady @MamaRachelRuto set for a State Visit to the U.S. on May 23, 2024, at the invitation of President Joe Biden and First Lady Jill Biden. https://t.co/rGCBqV9b7F
— Hussein Mohamed, MBS. (@HusseinMohamedg) February 16, 2024
SOMA PIA: Rais Ruto ametetea balozi wa marekani Meg Whitman dhidi ya matamshi ya kinara wa Azimio Raila Odinga