BY ISAYA BURUGU,29TH APRIL,2023-Rais  William Ruto ameapa kutumia kila nguvu  alizo nazo kuhakikisha kuwa  mandamano yaliyopangwa na mungano wa Azimio la Umoja one Kenya jumanne wiki ijayo  hayageuka na kuwa ghasia.Matamshi hayo ya Ruto yanafuatia  hatua ya Azimio kuazimia kurejelea mandamano yakitaiafa  kuhusiana na  kilichouita  kama kufeli kwa serikali kujitolea katika kufanikisha mazungumzo baina ya pande hizo mbili.

Akizungumza  huko Malava, kaunti ya kakamega hivi leo rais Ruto  amesisitiza kuwa  alimwendea kinara wa Azimio Raila Odinga akitaka suluhu ya kudumu kufikisha kikomo mzozo unaoendelea kati ya upinzani na serikali.

.Hata hivyo licha ya juhudi zake,rais amesema Raila ameonekana kukatalia  mbali nia yake na badala yake kuwaagiza wafuasi wake kushiriki mandamano.

Rais akiongeza kuwa lengo la serikali yake ni kuboresha Maisha ya wakenya na wala sio kukinzana na upinznani.

 

 

 

April 29, 2023