BY ISAYA BURUGU 6TH MAY 2023-Rais Wiliam Ruto  ni miongoni mwa wageni maarufu watakaohudhuria sherehe za kutawazwa kwa Mfalme Charles III wa Uingereza zinazofanyika hii leo.

Mke wa rais Joe Biden wa Marekani, Jill pia ni miongoni mwa wageni hao. Shughuli za uapisho zitafanyika Westminster Abbey na kuhudhuriwa na mamia ya viongozi wa mataifa mbalimbali na wageni walioalikwa kushuhudia Mfalme Charles na mkewe Camilla wakitawazwa kuwa mfalme na malkia.

Akiwa London, Jill atakutana na mke wa waziri mkuu Rishi Sunak, Akshata Murty katika makazi yao yaliyopo mtaa wa Downing na kutembelea ubalozi wa Marekani nchini humo na baadae kuhudhuria hafla iliyoandaliwa na mfalme katika kasri ya Buckingham.

Ingawa hakuna rais wa Marekani aliyewahi kuhudhuria shughuli hiyo, lakini hatua ya Biden ya kushindwa kuhudhuriwa imekosolewa pakubwa

 

 

 

May 6, 2023