BY ISAYA BURUGU 6TH APRIL,2023-Rais Wiliam Ruto hivi leo ameongoza uzinduzi wa ujenzi wa bwawa la Mwache katika wadi ya Kasemeni katika kaunti ndogo ya kinango kaunti ya Kwale.Muradi huo wa kima cha shilingi milioni 20  unatarajiwa kupiga jeki juhudi za kuwepo maji safi kwa  matumizi ya bidanamu na mifugo katika kaunti za Kwale na Mombasa.

Baada ya kukamilika, bwawa hilo linatarajiwa kuwa na uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo milioni 118 na usambazaji wa kila siku wa mita za ujazo 186000 za maji kwa kaunti za Kwale na Mombasa.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo rais amejitosa kwenye swala la kusaka suluhu kwa matakwa ya mungano wa Azimio la Umoja one Kenya kupitia bunge.

Rais amesisitiza kuwa bunge lina uwezo wakutosha kusuluhisha maswala yote ibuka na ni sharti lipewe fursa.

Rais aliyeonekana kuulenga upinzani amewasuta baadhi ya viongozi wakisiasa aliyowataja kama wenye kujitakia maslahi yao ya kibinafsi badala ya kushinikiza maslahi ya mwananchi.

Mungano wa Azimio kupitia kinara wake Raila Odinga ulisitisha mandamano yake ya kila juma wiki iliyopita kwa masharti kadha wa kadhaa ambayo ni sharti serikali ya Kenya Kwanza itimize.

Azimio wanataka,server za uchaguzi mkuu wa mwaka jana kufunguliwa,bei ya bidhaa muhimu na gharama ya kimaisha kurudi chini ,sawa  na kuanza upya mchakato wa kubuni tume ya uchaguzi kutumia mbinu ya kuwahusisha watu na makundi mbali mbali.

Akitangaza kusitisha mandamano na kutoa fursa kwa mazungumzo kati ya upinznai na serikali wiki iliyopita,Odinga alisema kuwa iwapo matakwa yao hayataanza kushughulikiwa katika muda wa juma moja basi hawatakuwa na la ziada bali kurejelea mandamano.

 

April 6, 2023