BY ISAYA BURUGU,28TH JUNE 2023-Rais  William Ruto amewaongoza wakenya katika kuwasilisha risala zake za kheri njema kwa  jamii ya waislam wanapoadhimisha siku kuu ya Idd-Ul-Adha.

Katika ujumbe ,rais amesisitiza umuhimu wa  siku ya leo akiwataka waumini wakislam kupokea kielelezo kutoka kwa maadili mema ya kujitolea,Imani na heshima  kwa mapenzi ya mwenyezi mungu.

Idd-Ul-Adha ni siku kuu muhimu yakidini  kwa waumini wakislam inayosherehekea kujitolea kwa nabii Abraham  kumtoa mwanawe wa pekee kama dhabihu kuwa heshima kwa Mungu.Waislam kote  duniani  wanaadhimisha siku kuu hii kwa shukrani,Imani na kujitolea

..Huanza kwa kusanyiko la sala   katika msikiti na maeneo ya wazi,ambapo waislam huvalia mavazi yao bora kwa ajili ya sala.

 

 

 

June 28, 2023