Taasisi husika katika wizara za kawi na ile ya barabara na uchukuzi, zimeagizwa kufutilia mbali kandarasi ya miaka 30 iliyokuwa imetolewa kwa kampuni ya Adani kupanua baadhi ya njia za umeme nchini.

Agizo hili limetolewa na rais William Ruto. Kwenye hotuba yake kwa taifa, rais Ruto pia ameagiza kusitishwa kwa makubaliano ya kuipa kampuni hiyo kandarasi ya kupanua uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA.

Uamuzi wa Ruto unajiri saa chache baada ya Marekani kufichua kuwa kampuni hiyo ya adani ilitumia ulaghai kupata kandarasi.

November 21, 2024