HAJI--OSOTUA-

Rais William Ruto ametangaza kumteua Noordin Haji, Mkurugenzi wa sasa wa Mashtaka ya Umma (DPP), kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS).

Taarifa rasmi iliyotiwa saini na Felix Koskei, Mkuu wa Utumishi wa Umma, ilieleza kuwa Haji atarejea katika kitengo cha Ujasusi, alikokuwa amehudumu hapo awali.

Iwapo uteuzi huu utaidhinishwa, Haji atatwaa wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu, akimrithi Meja Jenerali Mstaafu Philip Wachira Kameru, ambaye ameratibiwa kustaafu. Wakati hayo yakijiri, Rais Ruto bado hajamtangaza mrithi wa Haji katika nafasi ya Mkurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP)

May 16, 2023