Kiongozi wa Taifa Rais William Ruto amekutana na Rais wa Romania, Klaus Iohannis, ambaye alifika nchini kwa ziara rasmi ya siku tatu. Rais Iohannis na mkewe Carmen Johannis walipokelewa kwa heshima kubwa katika Ikulu ya Nairobi na Rais Ruto, Mama wa Taifa Bi. Rachel Ruto, pamoja na Naibu wa Rais Rigathi Gachagua na viongozi wengine wa serikali.
Katika siku zake za ziara, Rais Iohannis atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Ruto, pamoja na kufanya mkutano na Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira (UNEP) katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi. Ziara hii ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya Kenya na Romania katika masuala ya kidiplomasia, biashara, na maendeleo.
Rais Iohannis pia amepanga kufanya ziara katika nchi nyingine ya Afrika Mashariki, akiwa na mpango wa kutembelea Tanzania. Baadaye ataelekea Cape Verde na Senegal kwa mfululizo katika ziara zinazotarajiwa kukamilika tarehe 24 mwezi huu.
Kenya-Romania Media Briefing, State House, Nairobi. https://t.co/9o9o6glJ56
— William Samoei Ruto, PhD (@WilliamsRuto) November 14, 2023
Ziara ya rais huyu ni ishara muhimu wa ushirikiano wa kimataifa na uhusiano thabiti kati ya Romania na nchi za Kiafrika, baada ya taifa hilo kukubali kukoleza mahusiano na mataifa ya bara Afrika.