Rais Ruto

Rais William Ruto amesema yuko tayari kuongoza mazungumzo kati ya viongozi wakuu serikalini, wabunge na pia wale wa idara ya mahakama, ili kuimarisha juhudi za kukabiliana na ufisadi katika idara ya mahakama humu nchini.

Akizungumza katika eneo la Tinderet, Kaunti ya Nandi, kiongozi wa taifa amesema kwamba wakati umefika kwa taifa kuwa na mazungumzo na kukabiliana kikamilifu na ufisadi, ambao umesitisha miradi mingi ya maendeleo humu nchini.

Katika siku za hivi karibuni, viongozi wakuu serikalini wamekuwa wakiichimba idara ya mahakama, na kuisuta kwa kile walichokitaja kama kuhitilafiana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

January 16, 2024