Rais William Ruto ametangaza kuwa serikali itakomesha mahitaji ya viza kwa wageni wanaozuru nchini kutoka kote duniani kuanzia Januari 2024. Rais aliyasema haya wakati wa sherehe za miaka 60 za Jamhuri katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi.

Mkuu wa nchi alidokeza kuwa ukomeshaji wa mahitaji ya visa utafungua mipaka na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. Aidha alisema ili kutekeleza sera hii mpya, mfumo wa kidijitali umetengenezwa ili kuhakikisha kuwa wasafiri wote wanaozuru Kenya wanatambuliwa mapema kwenye jukwaa la kielektroniki. Kenya kwa sasa ni  nchi ya pili barani Afrika kufungua mipaka yake baada ya Rwanda kutangaza safari za bure kwa Waafrika wote. 

Kuhusiana na suala la uchumi, rais Ruto amewahakikishia wakenya kuwa nchi iko salama kutokana na hatari ya madeni huku akibainisha kuwa viegezo vyote vya kiuchumi vinaashiria habari njema ambapo mfumuko wa bei umeshuka hadi 6.8% kutoka 9.2% mwaka jana.

December 12, 2023