Rais William Ruto mapema hii leo alitia saini kuwa sheria mswada tata wa Fedha wa 2023, ambao ulipitishwa na Bunge la Kitaifa wiki jana.
Mswada huo ulipitia Bungeni baada ya kusomwa kwa mara ya tatu na Kuria Kimani ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango ya Kitaifa.
Wakenya sasa watalazimika kutumia fedha zaidi ili kufadhili bajeti ya kwanza ya serikali ya Kenya kwanza.
Miongoni mwa mapendekezo muhimu zaidi yaliyoidhinishwa kwenye mswada huo ni pamoja na ushuru wa ongezeko la thamani ya asilimia 16% kwenye bidhaa za petroli kutoka asilimia 8%.
Jumla ya wabunge 184 kutoka Kenya Kwanza -waliunga mkono mswada huo huku wabunge 88 kutoka Azimio wakiupinga.
πππππππππ ππππ πππππππ ππ π ππππππ ππππ ππππ πππ ππππππππππππππ ππππ ππππ
President @WilliamsRuto on Monday assented to the Finance Bill, 2023 and the Appropriations Bill, 2023 at State House, Nairobi.
He also⦠pic.twitter.com/vEos4D6GRG
β State House Kenya (@StateHouseKenya) June 26, 2023