Rais William Ruto hii leo ameliongoza taifa katika kuadhimisha siku kuu ya leba.
Akizungumza wakati wa hafla iliyoandaliwa katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi, rais Ruto amesema kuwa ako tayari kufanya kazi na viongozi wote wa miungano ya wafanyakazi kwa manufaa ya wakenya.
Rais vileile ameweka wazi kuwa serikali itatia saini mikataba itakayo wapa wakenya fursa ya kupata ajira katika mataifa mengine.
Hali kadhalika ameongeza kuwa Kenya inatazamiwa kupitisha sera kali ya malipo ambayo itakabiliana na gharama ya maisha.Chini ya mpango huo mpya, kima cha chini cha mshahara pia kitaongozwa na uendelevu na tija.
Kando na hayo amesema kuwa ana nia ya kuimarisha ustawi wa wafanyakazi na maslahi ya kazi ili kuongeza tija huku serikali ikiwa Β tayariΒ inapiga hatua katika kuimarisha haki za wafanyakazi nchini.
ππππππππππππ ππ πππ ππππ ππππ ππ ππππππ
Kenya is set to adopt a radical remuneration policy that will be responsive to the cost of living.
Under the new plan, the minimum wages will also be guided by sustainability and productivity.
Further,β¦ pic.twitter.com/4TeZdwRilu
β State House Kenya (@StateHouseKenya) May 1, 2023