Rais William Ruto kwa mara nyingine ametetea mfumo wa ufadhili wa elimu ya juu nchini.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kuhudumu kwa chuo kikuu cha Islamic humu nchini na chuo kikuu cha kitaifa cha ujasusi, rais Ruto amesema kuwa mfumo huo unahakikisha usawa katika elimu ya juu na pia kushughulikia changamoto za ufadhili katika vyuo vikuu.
Kando na hayo, aliiagiza tume ya elimu ya juu kuhakikisha viwango vya elimu vinazingatiwa kuambatana na mahitaji ya sekta hiyo.
Kwa upande wake, naibu rais Kithure Kindiki aliyehudhuria hafla hiyo, alikitaka chuo kikuu cha Islamic kulinda nchi dhidi ya uenezaji wa itikadi kali na utumiaji dini kwa njia isiyofaa kupitia dhana potovu.
Award of Charters to Islamic University of Kenya and National Intelligence and Research University, State House, Nairobi. https://t.co/bLAntlhEH4
— State House Kenya (@StateHouseKenya) November 5, 2024