Rais William Ruto yuko katika taifa jirani la Uganda, ambapo anatarajiwa kuwa miongoni mwa viongozi watakaohudhuria hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru katika taifa hilo. Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari, Rais Ruto aliondoka nchini adhuhuri ya leo na kupokelewa na rais wa Uganda Yoweri Museveni muda mfupi baadaye. Katika ziara yake, rais anatarajiwa kuandaa mazungumzo na mwenyeji wake kuhusu ushirikiano na kuimarisha uhusiano baina ya mataifa haya mawili.
Had a great meeting with President @KagutaMuseveni at @StateHouseUg, Entebbe, Uganda, ahead of tomorrow's 60th Independence Day celebrations. The Kenya - Uganda bond is growing stronger. pic.twitter.com/I8FvPBgUZC
— William Samoei Ruto, PhD (@WilliamsRuto) October 8, 2022
Ziara ya Rais Ruto imejiri siku kadhaa baada ya kauli ya mwanawe Rais Museveni Muhoozi Kainerugaba ambayo yalionekana kuzua mtafaruku wa kidiplomasia kati ya Kenya na Uganda. Katika mtandao wake wa Twitter, Muhoozi alichapisha jumbe akieleza kwamba angehitaji muda wa wiki mbili pekee kuuteka mji wa Nairobi. Kauli ambazo ziliibua hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya na Uganda na kumlazimu Museveni kuomba msamaha.