BY ISAYA BURUGU,11TH SEPT 2023-Mkenya mmoja kati ya 20 walio na umri wa kati ya miaka  15 na 65 wana uraibu wa pombe. Haya ni kwa mjibu wa utafiti KUHUSU hali ya matumizi ya mihadarati kwa kipindi cha mwaka 2022  uliyofanywa na halmashauri yakitaiafa dhidi ya mihadarat na pombe NACADA.

Ripoti hiyo imebaini kuwa wananchi kwa jumla wako kwenye hatari ya   kuingizwa katika utumizi wa dawa za kulevya katika umri  mdogo wa miaka 16.Umri wa chini kabisa mmoja kuingizwa katika matumizi ya sigara ni miaka sita,Pombe miaka saba na dawa zingine kati ya miaka minane na miaka 20.

Mutumizi ya sigara ndio maarufu Zaidi miongoni mwa wanafunzi wa shule za msingi,huku wanafuzni watano kati ya 15 wakitumia.Matumizi ya pombe yanafuata kisha miraa na Mugoka.

Hata hivyo miongoni mwa wanafuzni wa shule za upili nchini,pombe ndio inayotumiwa Zaidi,huku wanafunzi alfu 80 wakiripotiwa kutumia angalau asilimia 4 ya pombe.

Kwa ujumla vijana walio na umri wa miaka 15 hadi 24 hutumia miraa.Aidha ripoti hiyo imedokeza kuwa wafanyikazi wa sekta ya umma ndio walio na tatizo kubwa la utumizi wa pombe.Matumizi ya pombe miongoni mwa wafanyikazi wa sekta ya umma yakisimamia asilimia 23.8.

 

September 11, 2023