BY ISAYA BURUGU,22ND NOV,2023-Seneta wa Nandi Samson Cherargei hivi leo amefukuzwa nje ya Seneti wakati wa hafla ya Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen.

Katika video za  kikao hicho inamwonyesha Murkomen akijibu swali kuhusu fidia ya maskwota anaposimama na kisha spika, Seneta Abdulkadir Haji, akimtaka Cherargei kumpa Waziri huyo nafasi ya kujibu maswali yote.

Cherargei alipuuza uamuzi wa spika na kuendelea kusimama kinyume na sheria za bunge hilo huku Waziri Murkomen akiendelea kuzungumza.

Spika alilazimika  kukabili hali hiyo kwa mujibu wa sheria zinazo ongoza vikao vya bunge na kukatiza maelezo ya waziri Murkomen ya hali ya ujenzi wa Barabara ya Tala-Oldonyo Sabuk

.Hivi majuzi Cherargei ameonekana akimashambulia waziri Murkomen kwa maneno, kiasi cha kumtaka Rais William Ruto amwachishe kazi.

 

 

 

 

November 22, 2023