Rais William Ruto amesema kuwa utawala wake hautakopa pesa ili kuwalipa wafanyikazi wa umma mishahara yao.

Akizungumza katika hafla ya kutolewa kwa ripoti ya utendakazi wa idara za umma katika ukumbi wa KICC, Rais alieleza kwamba tatizo la kucheleweshwa kwa mishahara ya wafanyakazi wa umma limetokana na mikopo inayodaiwa na wakoeshaji wa nje.

Rais pia aliongeza kwamba hili ni tatizo ambalo limetokea kwa mara ya kwanza zaidi katika historia ya taifa la Kenya. Aidha rais aliweka bayana kwamba serikali haiku tayari kuchukua mikopo ili kukamilisha malipo yanayojirudia rudia kama vile mishahara, na badala yake kuongeza kuwa itafanya bidi ili kupata fedha zinazohitajika kutoka kwa wananchi.

Kauli ya Rais inajiri huku kukiwa na vitisho vya wafanyikazi wa serikali kususia kazi kushinikiza Hazina ya Kitaifa kutoa mishahara yao.

 

April 11, 2023