Serikali haitaongeza kandarasi za madaktari zilizotiwa saini kati ya Kenya na Cuba kufuatia kukamilika kwa mkataba huo mnamo Juni mwaka huu. Haya ni kwa mujibu wa waziri wa afya Susana Nakumicha.

Akifungua rasmi kongamano lililowaleta pamoja wadau wa afya, Nakhumicha alibainisha kuwa wafanyakazi wa ndani wana uwezo wa kutekeleza majukumu yanayotolewa na wenzao wa Cuba.

Kenya ilitia saini mkataba wa afya na Cuba mwaka wa 2017 ambao ulifanikisha mpango wa kubadilishana fedha ambapo madaktari wa Cuba wangekuja nchini kusaidia kujaza pengo katika hospitali za kaunti huku madaktari wa Kenya wakipelekwa Cuba kwa mafunzo maalum.

Aliongeza kuwa serikali inafanya kila iwezalo kutatua changamoto zinazokabili sekta hiyo ya afya haswa kuboresha mazingira ya kazi ya wahudumu wa afya.

 

October 11, 2023