BY ISAYA BURUGU 16TH JAN 2023-Wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na junior secondari mwaka huu hawatalipa karo yoyote .Haya ni kwa mjibu wawaziri wa elimu Ezekiek Machogu.Waziri akizungumza wakati wa kutangaza mikakati ya wanafuzni waliofanya KCPE mwaka jana kujiunga na shule za upili, amesema tayari serikali imetenga shilingi alfu 15000 kwa kila mwanafuzni kati ya wanafunzi Zaidi ya milioni moja wa gredi ya sita waliofanya mtihani wa KPSEA mwaka jana.
Waziri aliyezungumza na wandishi Habari katika taasisi ya ustawishaji mtaala nchini KICD jijini Nairobi, amesema ni shule zilizo na mabweni pekee ndizo zitakazoruhusiwa kudai karo ya muda hitaji hilo.Wakati huo huo , Machogu amesema serikali pia imepiga marufuku shule za upili za kiwango cha msingi kuitisha karo yoyote kwa watainiwa wa gredi ya saba.Waziri Machogu akichukua fursa hiyo kuondolewa mbali wasiwasi kuwa kuna uchache wawalimu watakaowafunza wanafunzi wa junior secondary.
. Zaidi ya wanafunzi milioni 1.2 waliofanya mtihani wa KCPE mwaka jana watatengewa fursa katika shule 112 za kitaiafa na 776 za extra county ,1,301 za kiwango cha kaunti na zingine 6,297 zilizo kwenye kaunti ndogo.Wengine watajiunga na shule 1,301 za sekondari za kibinafsi.Wanafunzi wanaweza kutuma ujumbe mfupi wa nambari yao ya usajili kwa nambari ya sms 22263 kufahamu shule ya upili watakayojiunga nayo.