Serikali itakarabati upya shule zilizosalia mahame katika maeneo ambayo hushuhudia mashambulizi ya mara kwa mara. Haya ni kwa mujibu wa waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki.

Waziri huyo alisema serikali imejitolea kufungua tena shule hizo kwa mujibu wa sera yake ya kuhakikisha upatikanaji sawa wa elimu kwa watoto wote. Alikuwa akizungumza katika Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Cheptuel, Eneobunge la Sigor, Kaunti ya Pokot Magharibi alipofanya tathmini ya usalama wa shule zilizotelekezwa ili kuwezesha kuanza kwa kazi za ukarabati kwa ajili ya kufunguliwa upya na kuanza tena masomo.

Vikosi vya Huduma ya Kitaifa ya Vijana (NYS) na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) vitashirikiana kukarabati angalau shule 50 katika kaunti za Baringo, Elgeyo Marakwet, Turkana, Pokot Magharibi, Samburu na Laikipia.

December 6, 2023