Rais William Ruto amesema serikali ina mpango wa kufanikisha kuondoa hitaji la visa kwa watalii na wageni wote wanaotaka kusafiri nchini, katika juhudi za kuimarisha utalii na kukuza ufahamu wa tamaduni za Kenya.
Akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya tamaduni ya jamii ya Turkana katika eneo la Lodwar, rais alifichua kuwa mpango huo unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.Hatua hii inalenga kuifanya Kenya kuwa kituo bora kwa watalii.
Kuondoa hitaji la visa kutaongeza urahisi wa kusafiri kuja humu nchini na kutoa fursa kwa ulimwengu kujifunza kuhusu utajiri wa tamaduni na desturi za Kenya. Kiongozi wa Taifa aidha amesema serikali kupitia wizara za utalii na tamaduni itaimarisha ufahamu wa wananchi kuhusu maswala ya tamaduni na desturi mbalimbali humu nchini.
Turkana Cultural and Tourism Festival (Tobonglore), Lodwar town. https://t.co/bUbNOdxuqA
— William Samoei Ruto, PhD (@WilliamsRuto) October 12, 2023