Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki hii leo amezuru kaunti za Mandera na Wajir ambapo amekutana na maafisa wakuu wa usalama katika kaunti hizo pamoja na Viongozi wa Jamii na wa kidini.

Kindiki amesema ushirikiano kati ya viongozi wa kidini na asasi za usalama utaangamiza magaidi  na kuwezesha maendeleo katika Mkoa wa Kaskazini Mashariki.

Aidha amefichua kuwa Serikali itatumia angalau Ksh.20B kuimarisha uwezo wa maafisa wa usalama katika mstari wa mbele kupitia uboreshaji wa vifaa vyao, teknolojia, na uwezo wa kukabiliana vilivyo na changamoto tata za usalama kama vile ugaidi na ujambazi.

Kando na hayo Kindiki ameahidi kuwa serikali itawashinda Al-shabaab na watu wote wenye msimamo mkali wanaoendelea kutishia usalama wa taifa na kuyumbisha jamii Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

July 4, 2023