ELIUD OWALO

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Eliud Owalo amesema serikali inajizatiti kuweka miundo-msingi bora na kutenga rasilimali za kutosha kuwekeza katika vituo 1450 vya kidijitali kote nchini kufanikisha mpango wa Jitume Youth Digital Empowerment.

Kwenye kikao na wanahabari baada ya kuzindua kituo sawia katika Chuo cha Kiufundi cha Kitale katika kaunti ya Trans Nzoia, Owalo amesema nia na madhumuni ya mpango huo ni kuujenga uchumi wa kidijitali.

Wakati huo huo mwenyekiti wa Kamati ya Teknolojia na Mawasiliano katika Bunge la Seneti  Allan Chesang na Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Wisley Rotich wamesema serikali itashirikiana na kampuni zingine kama vile Google, Amazon na Microsoft kufanikisha mradi huo.

https://twitter.com/EliudOwalo/status/1674010850636562433?s=20

June 28, 2023