Wizara ya mazingira na misitu nchini, kupitia idara ya ulinzi na uhifadhi wa misitu inapania kuzindua nambari za simu za bila malipo zitakazosaidia katika vita dhidi ya ukataji wa miti na uharibifu wa misitu katika maeneo tofauti ya taifa.
Akitangaza mipango hii Waziri wa mazingira nchini Sopian Tuya aliyehudhuria hafla ya upanzi wa miti katika msitu wa karura mapema leo, ameeleza kwamba wizara yake inakaza Kamba katika kuafikia lengo la upanzi wa miti Zaidi nchini, na wala hawatakubali yeyote kuhitilafiana na mipango hii.
Waziri Soipan aidha aliagiza idara ya ulinzi wa misitu kuanzisha mikakati kabambe ya kukabiliana na watu wanaoharibu misitu maeneo tofauti ya taifa, hasa misitu iliyo chini ya serikali akieleza kuwa misitu hii ndiyo iliyoathirika zaidi.
At a press briefing held at Karura Forest today, Cabinet Secretary Hon Soipan Tuya outlined the Ministry's key reforms in the management of forests, and directed Kenya Forest Service to mount an intensive, full scale operation to rid public forests of illegal activities. pic.twitter.com/oupUmMlVxk
— Ministry of Environment, Climate Change & Forestry (@Environment_Ke) May 5, 2023