BY ISAYA BURUGU 17TH MAY 2023-Serikali ya Canada imepuzilia mbali uumbe wa mtandao wa Twitter kutoka kwa Waziri wa maswala ya kigeni wa Kenya  Alfred Mutua kuwa kuna fursa chungu nzima za ajira kwa wakenya katika taifa hilo la magharibi mwa Marekani.

Idara ya uhamiaji,wakimbizi na uraia ya Canada  imetaja ujumbe huo wa Mutua kama unaopotosha.Idara hiyo badala yake imewataka wakenya  na watu walio na nia ya  kuhamia nchini Canada  kuhakikisha kuwa wanapokea Habari zinazofaa kupitia kutembelea tuvuti yake  ya http://Canada.ca/immigration.

Hiyo jana Jumane Mutua alisema serikali ya Kenya ilikuwa imeafikia makubaliano na serikali ya Canada kuwapa fursa za ajira wakenya.Wakati wa ziara ramsi nchini Canada ,Waziri Mutua alitanagza Habari hizo kupitia akaunti yake ya mtandao wakijamii wa Twitter.

Mutua alidai kuwa alikuwa amefanya mazungumzo na mwenzake wa Canada  kuhusu fursa za ajira kwa wakenya katika taifa hilo.

 

 

 

 

 

May 17, 2023