Wakenya wapatao 240,000 katika kaunti ya Narok wanakumbwa na makali ya njaa baada ya kushuhudiwa kwa vipindi virefu vya jua na ukame unaokumba kaunti 23 kote nchini. Ni kutokana na hali hii ambapo viongozi wa serikali ya kaunti ya Narok wakiongozwa na gavana Patric Ole Ntutu pamoja na viongozi wa sekta mbalimbali katika kaunti ya Narok wameanzisha juhudi za kuwasaida wananchi kukabiliana na makali ya njaa. Gavana Ntutu pamoja na kamishena wa Narok Bw.Isaac Masinde wameongoza kikao cha kujadili mbinu mwafaka za kuwasaidia wananchi walio katika hatari zaidi.

Akiwahutubia waandishi wa habari nje ya Ofisi yake kamishena Isaac Masinde amesema zaidi ya shule 130 katika kaunti ya Narok zinahitaji msaada wa chakula kutokana na makali ya njaa. Masinde amesema kuwa serikali kwa ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali wanafanya juhudi  za pamoja ili kuhakikisha kuwa wamesamabaza chakula cha msaada kwa maeneo yaliyoathirika. 

Gavana Ntutukwa upande wake amesema kuwa sehemu zilizokabwa zaidi na njaa ni maeneo ya Mosiro Narok mashariki, Narosura, maji moto, eneo la Loita, Naikara, kapsasian eneo la Ilkeren Trasmara magharibi pamoja na eneobunge la Emurua Dikirr. Ntutu amesema serikali ya kaunti ya Narok itashirikiana na ile ya kitaifa kuhakikisha kuwa misaada mbali mbali imewafikia wakazi wa maeneo haya. 

Taarifa zaidi

Marekani Yasitisha Ufadhili wa Umoja wa Mataifa kwa Operesheni Haiti.

Serikali ya Marekani imetangaza kusitisha ufadhili wake kwa operesheni ya Umoja wa Mataifa inayolenga kurejesha utulivu nchini Haiti.…

SUSWA | Mafisa wa Polisi Wapewa Makataa ya Siku Tano Kuhama Eneo Hilo.

Mafisa wa polisi katika eneo la Suswa, Narok Mashariki, wamepewa hadi siku tano kuhama baada ya makabiliano makali…

Wanachama wa kamati ya kuwateua makamishna wa IEBC waapishwa.

Wanachama wa kamati iliyoteuliwa na rais William Ruto asubuhi ya leo kuwapiga msasa na kuwateua makamishna wa IEBC…

October 11, 2022