Serikali ya kaunti ya Narok inapana kuwaajiri watu 700 mwaka huu katika idara mbali mbali za serikali. Haya ni kwa mujibu wa gavana wa Narok patrick Ntutu.

Akilihutubia bunge la kaunti ya Narok wakati wa hfala ya kuapishwa kwa afisa mkuu mtendaji wa idara ya kilimo katika serikali ya Narok Biarose Chemutai pamoja na mwanachama wa bodi ya utumishi wa umma ya Narok Mercy Netaya Pion, gavana Ntutu ameeleza kuwa hatua hiyo pia inalenga kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi wa kaunti ya Narok.

Kwa upande wake spika wa bunge la kaunti ya Narok Devis Dikirr amewapongeza maafisa hao wapya huku  akiwataka kufanya kazi bila ubaguzi wowote.

January 13, 2025

Leave a Comment