Msemaji wa serikali Isaac Mwaura amesema kwamba hatua ya Marekani kusitisha ufadhili wake wa shilingi bilioni 1.71 kwa shirika la umoja wa mataifa UN, kwenye operesheni ya kurejesha utulivu nchini Haiti,haitaathiri kwa namna yoyote operesheni hiyo.

Kupitia taarifa, Mwaura amesema kwamba misheni hiyo pia inafadhiliwa na hazina maalum ambayo iliundwa Oktoba mwaka wa 2023 na UN ili kushugulikia mzozo wa Haiti huku akieleza kuwa misheni hiyo inajumuisha pia maafisa wa polisi kutoka mataifa mengine kama vile Jamaica, Guatemala na Bahamas miongoni mwa mengine.

Taarifa ya Mwaura imetiliwa mkazo na mshauri wa rais katika masuala ya usalama Monica Juma, ambaye amesema kwamba operesheni hiyo itaendelea kuungwa mkono na takriban dola milioni 110 kutoka kwa wafadhili wengine.

February 5, 2025

Leave a Comment