Ukarabati wa Barabara Narok

Serikali ya Kaunti ya Narok imetangaza mafanikio katika ukarabati wa barabara mjini Narok, huku jumla ya kilomita 42 zilkiwa zimekarabatiwa. Hatua hii inalenga kupunguza changamoto njia mbovu ambazo zimekuwa tatizo kubwa katika maeneo mengi ya mji wa Narok.

Waziri wa Barabara katika Kaunti ya Narok, John Gatua, ndiye aliyesema haya kupitia kwa mawasiliano kwa njia ya  simu katika kipindi cha Osotua Express kinachopeperushwa na idhaa ya Radio Osotua. Gatua aliahidi kuwa juhudi za ukarabati zitaendelea kufanyika katika maeneo mengine ya Narok kama vile Olokurto, Olposimorou, Melili, na Nkareta, na lengo lao ni kukamilisha ujenzi huu ndani ya mwezi mmoja, kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua kulingana na taarifa kutoka idara ya utabiri wa anga.

Waziri John Gatua Narok
Waziri wa Barabara wa Kaunti ya Narok John Gatua, akizungumza katika hafla iliyopita.
PICHA: Narok County Governnment (X)

SOMA PIA:Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu apokea ripoti ya ukaguzi wa ofisi ya HR na Mishahara.

Gatua pia alifafanua kuwa gharama kubwa za ujenzi wa barabara za kudumu zimewalazimu kufanya marekebisho  kwa sasa, ili kukabiliana na matatizo ya muda ambayo yamekuwa yakisumbua wananchi wa Narok mjini. Wananchi wamekuwa wakipata shida kubwa kutokana na barabara mbovu, hususan wakati wa mvua kubwa ambazo zimekuwa zikinyesha tangu mwishoni mwa mwaka uliopita.

 

February 6, 2024