Akina mama ambao ni wakulima wa maziwa katika eneo la Olorropil kwenye kaunti ndogo ya Narok kaskazini wametoa wito kwa serikali ya Narok kuweka mikakati itakayosaidia kuimarisha biashara ya maziwa eneo hilo.
Kwa mujibu wa kina mama hao ni kwamba kwa sasa wanalazimika kuuza kila lita ya maziwa kwa shilingi 35 bei ambayo wanasema ni duni huku wakidai kutopata faida yoyote ya bidhaa hiyo.
Kando na hayo wameongeza kwamba kulinda afya ya mifugo na kuhakikisha wanapata malisho na maji bado wanategemea mapato hayo ambapo wanasema sasa inakuwa vigumu kwao.Wamesisitiza haja ya serikali kuingilia kati swala hilo ili angalau kuimarisha bei ya bidhaa hiyo waweze kujiimarisha kiuchumi.