Serikali ya Kenya imeahidi kuendelea kumpigia debe kinara wa azimio la umoja Raila Odinga kwenye kinyang’anyiro cha uenyekiti wa muungano wa umoja wa Afrika huku uchaguzi ukiratibiwa kufanyika mwezi Februari mwaka ujao. Haya yamewekwa wazi na mkuu wa baraza la mawaziri nchini Musalia Mudavadi.

Akiwahutubia waandishi wa habari walipokuwa wakitoa taarifa ya pamoja,Musalia amesema kuwa uzoefu wa Odinga kwenye masuala ya kisiasa na uongozi utamwezesha kutaua changamoto zinazokumba bara la Afrika

Kwa upande wake Odinga, ameshikilia kwamba ana ujuzi wa kutosha wa kuipeleka AU katika hatua nyingine na kufichua kuwa marafiki wake ndio walimshinikiza kuwani kiti hicho cha AU.

Itakumbukwa kuwa Odinga amekuwa akifanya ziara katika mataifa mbalimbali barani Afrika ili kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wakuu wa mataifa hayo. Uenyekiti huo wa AU umewavutia wagombea 4 kwa ujumla kutoka mataifa ya Kenya, Somalia, Djibouti na Seychells.

June 5, 2024