Serikali itashughulikia mara kwa mara changamoto zinazoendelea za rasilimali watu na zinazopunguza kasi ya kutimizwa kwa mpango wa Huduma ya Afya kwa Wote UHC.

Akizungumza alipokutana na viongozi wa muungano wa madaktari KMPDU katika ikulu ya rais,Ruto alisema serikali itaendelea kuwashirikisha wadau katika sekta ya afya, vikiwemo vyama vya wafanyakazi wa afya, ili kukuza maelewano ya viwanda na kutatua changamoto za kudumu kwa muda mrefu.

Kwa upande wake katibu wa muungano huo Davji Atellah ameelezea kujitolea kwa muungano huo kuunga mkono UHC sawa na kupigia debe bima ya afya ya jamii SHIF.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ni mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Kosgei, waziri wa Afya Susan Nakhumicha na Katibu wa Afya ya Umma Mary Muthoni.

May 11, 2024