Rais William Ruto amesema serikali yake iko tayari kushirikiana na kuunga mkono taasisi za elimu ya juu ili kuimarisha uwezo wao wa kiufundi.
Akizungumza katika Chuo Kikuu cha TUK ambapo alizindua majengo ya masomo, Ruto amesema serikali yake itaunda mfumo utakaowezesha kila chuo kikuu kudahili wanafunzi ambao serikali inaweza kufadhili.
PRESIDENT RUTO: TECHNICAL TRAINING WILL DRIVE OUR ECONOMIC GROWTH
The Government will work with tertiary institutions to forge a pathway for Kenya to deepen its competitive technical capacity. pic.twitter.com/mRppAARE7x
— State House Kenya (@StateHouseKenya) December 8, 2022
Wakati wa kampeni, Ruto aliahidi kushughulikia changamoto zinazokumba taasisi za elimu ya juu kwa kutoa fedha zaidi ili kuendeleza shughuli zao ikizingatiwa kwamba vyuo vikuu vyote vimetengewa asilimia 50 pekee ya fedha zinazohitajika kuviendesha.
Kwa upande wake waziri wa elimu Ezekiel Machogu aliyehudhuria hafla hiyo amesema kuwa kuanzia mwaka ujao wanafunzi wanaosemea kozi za diploma pia watapata ufadhili kutoka kwa serikali kupitia fedha ambazo hutolewa kwa wanafunzi na serikali yaani capitation fee.