BY ISAYA BURUGU,3RD AUG 2023-Serikali imedhibitisha kuwa muradi wa sarafu kidigitali ya Worldcoin, ambayo oparesheni zake zimesitishwa humu nchini haujasajiliwa kisheria nchini Kenya.
Kupitia taarifa ya Pamoja iliyotolewa na wizara za usalama wa ndani sawa na ile ya teknologia ya mawasiliano ya ICT ,imetoa ufichuzi huo ikijibu swali lililoibuliwa na mbunge wa Manyatta John Mukunji bungeni hiyo jana.
Kwa mjibu wa serikali ,kampuni hiyo ya kigeni ilikabidhi huduma zake za kukusanya data kwa kampuni ya humu nchini iliyotambuliwa kama Sense Marketing, iliyokuwa ikikusanya maelezo kutoka kwa wakenya huku ikiwalipa shilingi alfu saba.
Mkuruygenzi mkuu wa idara ya upelelezi nchini DCI hiyo jana aliwanasa maafisa wawili wa kampuni ya Worldcoin humu nchini na sasa wanawasaidia makachero kwa uchunguzi kuhusu muundo na oparesheni za sarafu hiyo.
Wawili hao ni Emmanuel Otieno, anayesemekana kuwa mkuu wa oparesheni na Rael Mwende ambaye ni meneja wa kampuni hiyo humu nchini.